Halmashauri ya wilaya ya kondoa ina miliki msitu mkubwa wa Isabe(Isabe Local Authority Forest Reserve) wenye ukubwa wa hekta 4249, misitu hii huanzia katika safu za milima kolo katika kijiji cha kolo hadi kijiji cha bukulu kata ya soera.Pia kuna misitu ya jamii hii ni misitu ambayo iko chini ya halmashauri za vijiji, hii inahusisha vijiji vya Kisese sauna ,Mitati ,Mkurumuzi, kikore na Madege.Pamoja na kua chini ya halmashauri za vijiji lakini pia inasimamiwa na halmashauri kwa sheria ya misitu ya mwaka 2009 na sheria ndogo za halmashauri lengo na madhumuni ni kutunza vyanzo vya maji na mazingira kwa ujumla.Shughuli za kibinadamu kama kilimo ,ukataji mkaa na ufugaji ni marufuku kufanyika katika maeneo haya.
KONDOA DISTRICT COUNCIL ,BUKULU VILLAGE
Anuani ya Posta: Box 1 Kondoa
Simu : 0262360313
Simu ya Kiganjani:
Barua Pepe: info@kondoadc.go.tz na ded@kondoadc.go.tz
Hakimiliki ©2017 Halmashauri ya Wilaya ya Kondoa . Haki zote zimehifadhiwa.